Walioathirika na virusi vya ukimwi kisiwani Nkombo wanaiomba serikali au wahisani kuwapatia msaada wa chakula ili kiwasaidie kuwawezesha ku mudu maisha yawo kutokana na tatizo walilo nalo la kushindwa kutumia dawa za kupunguza makari ya virusi vya ukimwi liweze kutaturiwa.

Haya yalitangazwa na waathirika wa virusi vya kuambukiza ukimwi katika Kata ya Nkombo wilayani Rusizi mkoa wa Magharibi kwenye mahojiano na waandishi wa habari za Afya walioko kwenye jumuia ya kupambana na magonjwa zaidi wakijikita na ugonjwa wa ukimwi kama ABASIRWA.
Katika mahojiano hayo ambayo yaliwakutanisha baadhi ya waathirika kisiwani humo kwenye kituo cha afya cha Nkombo kwanza walianza wakishukuru serikali kwa namna inavyo jali waathirika kwa kuwapatia dawa za kufubaza virusi hiyo bila maripo rakini pamoja na hayo wakadai kuwa bado wanahitaji msaada zaidi.
Mmoja wa waathirika hao mzee wa umri wa miaka 81 amabaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kwa niaba ya wenzake kuwa wanapotumia hizo dawa ARVs husikia kizunguzungu kutokana na nguvu dawa hizo zilizo nazo ukiringanisha na miili yawo amabayo iliyodhofika kwa kukosa kinga kutokana na ukosefu wa chakula cha kutosha hivo baadhi yao wanaamua kutotumia dawa hizo.
Alisema kuwa ukitumia dawa hizo za ARV bila kula chochote mwili unachoka na huwezi kufanya kazi yoyote ya nguvu na ndiyo maana tunaomba tusaidiwe anagalawu chakula au unga wa uji ili tuweze kusukuma maisha.
Huu uhaba wa chakula kisiwani humo ulithibitishwa na afisa ustawi wa jamii wa kata hiyo Bwana Evariste Ngendahayo wakati akieleza sura halisi ya kata anayoongoza.
Alisema kata hiyo ya Nkombo imekariwa na wakazi 21,762 kwenye eneo la mraba km 29 ambazo km 7 ni maji zilizo baki km 22 ndiyo ardhi ambayo haitoshi ukiringanisha wakazi wenyewe.
Ardhi yenyewe ni ndogo isitoshe na udongo wake hauna rutuba inabidi mkulima ilia apate mazao atumiye mbolea ya chumvi chumvi ambapo si kila mwananchi ana uwezo wa kuinunua kwa sababu vipato vyao ni kidogo sana, hiyo ndiyo asili ya uhaba wa chakula kisiwani humo. Alinukuliwa akisema.
Afisa huyo aliendelea kusema kuwa hata wafanya biashara ni wachache na biashara zao ndogo ndogo nazo zinatoka nchi ya jirani akiwa na maana ya Jamuhuri ya kidemokarasi ya Kongo (RDC) ambako wengine wana amua kuhamia huko huko.
Muganga musimamizi wa kituo cha afya kisiwani humo Bwana Francois Xavio Ntakirutiman
Kutokana taarifa ya muganga musimamizi wa kituo cha afya kisiwani humo Bwana Francois Xavio Ntakirutimana aliwambia waandishi wa habari kuwa katika kata hiyo waishio na virusi amabao hupata dawa kituoni hapo ni jumla ya watu 107 na kati yao 66 ni wanaume na wanawake ni 41 na hii ni kuanzia miaka 17 na wanaopewa dawa za miezi 6 ni 46.
Alipoulizwa kuhusu ukahaba alisema kuwa kisiwani humo hakuna ukahaba, akiwa na maana ya wale wasichana au akina mama wauzao miili yao hakuna
umwezi.rw

